Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) - ABNA - Swala ya Ijumaa imeswaliwa Leo hii 25.04.2025 huko (NUNGE) DODOMA katika Masjid ya Ahlu-Sunna. Imam wa leo ni Naibu Kadhi Mkuu na Mjumbe Baraza la Ulamaa BAKWATA Taifa Sheikh Ali Ngeruko.
Swala ya Ijumaa Masjid Nunge - Dodoma
Mh. Waziri Abdallah Ulega pamoja na mwenyekiti wa Masjid Sunni (Nunge) alhaj Ismail Dawood na katibu wa Sektetarieti ya Baraza la Ulamaa pamoja na Afisa Ofisi ya Mufti Makao Makuu, Alhaj Hotty nao wamehudhuria pamoja na waumini waliofurika kwenye Msikiti huo.
Baada ya Swala, Alhaj Ismail Dawoud alikabidhiwa barua ya kuteuliwa kuwa Mshauri maalum wa Mufti wa Tanzania.
Ripoti hii ni kwa hisani kubwa ya:
Dr. Harith Nkussa
Msemaji Maalum wa Mufti
Ijumaa 25.4.2025.
Dodoma
Your Comment